15 - Nena Mungu

15 - Nena Mungu
"Speak To My Soul"

1.

Nena rohoni Yesu, Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo, "Huachwi upweke."
Fungua moyo wangu, Nisikie mara;
Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.

Kila siku unene, Vile kwa upole,
Nong`oneza kwa pole wa pendo:
"Daima utashinda, Uhuru ni wako."
Nisikie maneno; "Huachwi upweke."


2.

Nena kwa wana wako, waonyeshe njia, 
Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa Maisha kamili,
Wahimize ufalme, Tumwone mwokozi.

3.

Nena kama zamani, Ulipoitoa
Sheria takatifu: Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mapenzi yoko tena, Daima kusifu.
 
(Amina)

Comments

Popular posts from this blog

06 - Kumekucha Kwa Uzuri

05 - Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu

02 - Twamsifu Mungu