Posts

Showing posts from April, 2023

01 - Mtakatifu, Mtakatifu,Mtakatifu

01 - Mtakatifu, Mtakatifu,Mtakatifu "Holy, Holy, Holy" 1. U Mtakatifu! Mungu mwenyezi! Alfajiri sifa zako tutaimba; U Mtakatifu , Bwana wa huruma, Mungu wa vyote hata milele. 2. U Mtakatifu! Na malaika Wengi sana wanakuabudu wote; Elfu na maelfu wanakusujudu Wa zamani na hata milele. 3. U Mtakatifu! Ingawa giza Lakuficha fahari tusiione, U Mtakatifu! Wewe peke yako, Kamili kwa uwezo na pendo. (Amina)  

02 - Twamsifu Mungu

02 - Twamsifu Mungu "We Praise Thee, O God" 1. Twamsifu Mungu, Mwana wa upendo Aliyetufia na kupaa juu. Aleluya! Usifiwe, Aleluya! Amin; Aleluya! Usifiwe, utabariki. 2. Twamsifu Mungu, Roho mtakatifu, Akatufunulia Mwokozi wetu. 3. Twamsifu Mwana, aliyetufia Ametukomboa na kutuongoza. 4. Twamsifu Mungu wa neema yote Aliyetwaa dhambi, akazifuta. 5. Twamshe tena, tujaze na pendo. Moyoni uwashe moto wa Roho. (Amina)

03 - Mungu Atukuzwe

03 - Mungu Atukuzwe "To God Be The Glory" 1. Mungu atukuzwe kwa mambo makuu,  Upendo wake ulitupa Yesu, Aliyejitoa maisha yake, Tuwe nao uzima wamilele. Msifu, msifu, dunia sikia; Msifu, msifu, watu wafurahi; Na uje kwa Baba, kwa yesu Mwana, Ukamtutukuze kwa mambo yote. 2. Wokovu kamili, zawadi kwetu, Ahadi ya Mungu kwa ulimwengu; Wanaomwamini na kuungama, Mara moja wale husamehewa 3. Alitufundisha mambo makuu,  Alihakikisha wokovu wetu, Lakini zaidi, ajabu kubwa, Yesu atakuja na tutamwona.  (Amina)

04 - Jina LA Yesu Salamu

04 - Jina LA Yesu Salamu "All Hail The Power" 1. Jina la Yesu, salamu! Lisujidieni, Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni 2. Enzi na apewe kwenu, watetea dini; Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni 3. Enyi mbegu ya rehema nanyi msifu; Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni 4. Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni. 5. Kila mtu duniani msujudieni Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni. 6. Sisi na wao pamoja tu mumo sifani. Milele sifa ni moja, na `mpeni` Milele sifa ni moja, na `enzi mpeni`   (Amina)

05 - Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu

05 - Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu "O Worship The King" 1. Na tumwabudu  huyu Mfalme, Sifa za nguvu zake zivume; Ni ngao, ni ngome, Yeye milele, Ndizo sifa zake kale na kale. 2. Tazameni ulimwengu huu, Ulivyoumwa, ajabu kuu; Sasa umewekwa pahali pake, Hata utimize majira yake. 3. Kwa ulinzi wako, kwetu Bwana, Twakushukuru, U mwema sana; Hupewa chakula kila kiumbe, Kila kitu kila mahali pake. 4. Wanadamu tu wanyange sana, Twakutumaini wewe, Bwana; Kamwe haupunguiwsako wema, Mkoombozi wetu, Rafiki mwema.   (Amina)

06 - Kumekucha Kwa Uzuri

 06 - Kumekucha Kwa Uzuri "The Morning Bright Rosy' 1. Kumekucha kwa uzuri. Nafumbua macho; Baba amenihifadhi, Ni wake moto. 2. Bwana niwe leo kutwa Ulinzini mwako; Nisamehe dhambi, niwe Mikononi mwako. 3. Roho wako anikae moyoni daima; Anitakase, nione Uso wako. (Amina)

07 - Mungu Msaada Wetu

 07 - Mungu Msaada Wetu "O God Our Help In Ages" 1. Mungu Msaada wetu tangu miaka yote; Ndiwe tumaini letu la zamani zote. 2. Kivuli cha kiti chako ndiyo ngome yetu, Watosha mkono wako ni ulinzi wetu. 3. Kwanza havijakuwako nchi na milima, Ndiwe Mungu; chini yako twakaa salama. 4. Na miaka elfu ni kama siku moja kwako; Utatulinda daima, tu wenyeji wako. 5. Bwana msaada wetu tangu miaka yote, Mlinzi wetu na ngome, daima, milele. (Amina)

08 - Uje Ukombozi

08 - Uje Ukombozi "O Hear My Cry" 1. Unisikie ninapolia, Uje. M-kombozi; Moyo wangu hukutazamia, Uje. M-kombozi. Nimepotea mbali na kwangu, Nimetanga peke yangu; Unichukulie sasa kwako: Uje M-kombozi. 2. Sina pahali pa kupumzika, Uje M-kombozi Unipe raha, nuru, uzima, Uje M-kombozi. 3. Nimechoka, njia ni ndefu Uje, M-kombozi Macho yako kuona nataka, Uje M-kombozi. 4. Bwana daima hutanidharau, Uje, M-kombozi Kilio changu utanijibu, Uje, M-kombozi. (Amina)

09 - Mwumbaji , Mfalme

  09 - Mwumbaji , Mfalme "My Maker And My King" 1. Mwumbaji, Mfalme, Vitu vyote vyako; Ni kwa ukarimu wako; Ninabarikiwa, Ni kwa ukarimu wako, Ninabarikiwa. 2. Uliyeniumba, Nakutegemea; Sina budi kuzisifu Hisani zako kuu, Sina budi kuzisifu Hisani zako kuu. 3. Nitatoa nini? Kwanza vyote vyako, Upendo wako wadai Moyo wa shukrani, Upendo wako wadai Moyo wa shukrani. 4. Nipewe neema, Niwe na uwezo Wa kuishi kwako, Bwana: Siku zangu,zako, Wa kuishi kwako, Bwana: Siku zangu,zako. (Amina)

10 - Kristo Wa Neema Yote

 10 - Kristo Wa Neema Yote     "Come Thou Fount" 1. Kristo wa neema zote imbisha moyo wangu Mifulizo ya Baraka inaamsha shangwe kuu. Unifunze nikupende, nikuandame kote, Moyo wangu ukajaefuraha na tumaini. 2. Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku. Salama aniongoza hata kule nyuumbani. Yesu alinitafuta njiani mbali kwake, Akatoa damu yake nipone hatarini. 3. Kweli mimi mwiwa mkubwa wa neema daima; Wema wako unifunge zaidi kwako Bwana. Ili nisivutwe tena kukuacha, ee Mponya, Nitwalie moyo wangu uwe wako kamili. (Amina)

11 - Jina La Bwana Li Heri

11 - Jina La Bwana Li Heri "O For A Thousand Tongues To Sing" 1. Sauti zote ziimbe, jina la Yesu li heri ! Sifa za mfalme Mungu, jina la Yesu li heri ! Jina li heri, jina li heri, jina la Yesu li heri. Jina li heri, jina li heri, jina la Yesu li heri 2. Hofu zote la tuliza, jina la Yesu li heri ! Mwenye dhambi hukubali, jina la Yesu li heri. 3. Huvunja nguvu za dhambi, jina la Yesu li heri. Damu yake hutakasa, jina la Yesu li heri. 4. Sauti yake ni tamu, jina la Yesu li heri. Wakaburini husikia, jina la Yesu li heri. 5. Lugha maelf(u) zitaimba, jina la Yesu li heri. Astahili Mwana-Kondoo,  jina la Yesu li heri.   (Amina)

12 - Msifu Mungu

12 - Msifu Mungu "Praise God From Whom All Blessings Flow" 1. Msifu Mungu wa neema, Enyi viumbe po pote; Wa juu pia sifuni Baba, Mwana naye Roho! Amin!  (Amina)

13 - Yesu Uje Kwetu

13 - Yesu Uje Kwetu "Jesus Thou Hast Promised" 1. Umetuahidi kwamba wawili watatu , Kwajina lako wakija, Utabariki; Kwa hivi leo twapiga magoti nyumbani pako. Yesu uje kwetu Utubariki; Yesu uje kwetu Uwe karibu. 2. Umekuwa nasi siku nyingine, Tunakuhitaji mpaka mwisho. Uje Mwokozi, tupe neema; ‘Tusikie Yesu, utubariki. 3. Uje utawale sauti zetu: Nyimbo, nazo sala uziagize; Imani izidi, ikamilike; Pendo liwe safi, na njia nuru.   (Amina)

14 - Nitembee Nawe

 14 - Nitembee Nawe "O Let Me Walk With Thee" 1. Nitembee nawe mungu Alivyo tembea Henok; Mkonop wangu uushike: Unene nami kwa pole; Ingawa njia siioni, Yesu nitembee nawe. 2. Siwezi tembea pekee: pana dhoruba mbinguni; Mitego ya miguu, elfu; Adui wengi hufichwa; Uitulize bahari, Yesu nitembee nawe. 3. Ukinishika mkono Anasa kwangu hasara; Kwa nguvu nitasafiri; `Tautwika msalaba; Hata mji wa Sayuni Yesu nitembee nawe. (Amina)

15 - Nena Mungu

15 - Nena Mungu "Speak To My Soul" 1. Nena rohoni Yesu, Nena kwa upole Sema kwangu kwa pendo, "Huachwi upweke." Fungua moyo wangu, Nisikie mara; Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana. Kila siku unene, Vile kwa upole, Nong`oneza kwa pole wa pendo: "Daima utashinda, Uhuru ni wako." Nisikie maneno; "Huachwi upweke." 2. Nena kwa wana wako, waonyeshe njia,  Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba; Wajifunze kutoa Maisha kamili, Wahimize ufalme, Tumwone mwokozi. 3. Nena kama zamani, Ulipoitoa Sheria takatifu: Niiweke pia; Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu, Mapenzi yoko tena, Daima kusifu.   (Amina)

16 - Ninakuhitaji

16 - Ninakuhitaji "Blessed Lord, How Much I Need Thee" 1. Bwana ninakuhitaji! Nimpofu, maskini; Unishike mkononi, Kwako napata nguvu. Kila saa, kila saa Bwana ninakuhitaji; Kila saa, kila saa, Unilinde kila saa. 2. Univike na mavazi Ya usikivu wako; Nguo zangu ni machafu, Nazitamani zako. 3. Wewe ukiniongoza Nitakwenda salama; Nenda nami siku zote, U nuru na uzima. 4. Na ikiwa m-beleni Sehemu yangu ngumu, Au ikiwa furaha, Unilinde kila saa. (Amina)

17 - Si Mimi, Kristo

17 - Si Mimi, Kristo "Not I But Christ" 1. Si mimi, Kristo astahili sifa; Si mimi, Kristo ajulikane; Si mimi, Kristo katika maneno Si mimi, Kristo kwa kila tendo 2. Si mimi, Kristo, kuiponya huzuni; Kristo pekee, kufuta machozi; Si mimi, Kristo, kubeba mzigo; Si mimi, Kristo, hupunga hofu. 3. Kristo pekee, pasipo kujisifu; Kristo pekee, na nisizungumze Kristo pekee, na hakuna kiburi; Kristo pekee, sifa yangu ife. 4. Kristo pekee, mahitaji atoe Si mimi, Kristo, kisima changu; Kristo pekee, kwa mwili na kwa moyo. Si mimi, Kristo, hata milele.   (Amina)

18 - Mwokozi, Kama Mchunga

 18 - Mwokozi, Kama Mchunga "Saviour, like A Shepherd 1. Mwokozi, kama mchunga Utuongoze leo; Ututume malishoni; Fanya tayari boma. Bwana Yesu, peke yako Umetuvuta kwako. 2. Tu wakouwe rafiki, Uwe mlinzi wetu; Kundi lako ulilinde, Tusivutwe na dhambi; Bwana Yesu, tusike, Tukiomba, samehe. 3. Umetuahidi kwamba Utakubali watu, Utawahurumia na Utawapa neema; Bwana Yesu, tunapenda kuwa wako, mapema. (Amina)

19 - Msalabani Pa Mwokozi

19 - Msalabani Pa Mwokozi     "Down At The Cross" 1. Msalabani pa Mwokozi Hapo niliomba upozi, Moyo wangu ulitakaswa, Na asifiwe. Na asifiwe, Na asifiwe, Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe. 2. Chini ya mti msumbufu Niliomba utakatifu, Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe. 3. Kwa ajabu nina okoka, Yesu anakaa moyoni; Mtini alinifia, Na asifiwe. 4. Damu ya Yesu ya dhamani Huniokoa makosani; Huniendesha wokovuni, Na asifiwe.  (Amina)

20 - Mungu Wetu Yeye Mwamba

20 - Mungu Wetu Yeye Mwamba    "The Lord's Our Rock" 1. Mungu wetu yeye mwamba, Kimbilio taabuni; Msaada penye shida ulio karibu sana. Mwambna wetu kutupumzisha, yu kivuli kuburudisha  Yu Mwongozi katika njia, kimbilio taabuni. 2. Mchana usiku, yule kimbilio taabuni, Hivyo hatutaogopa, kwani yu karibu sana. 3. Iwayo yote, Yeye tu kimbilio taabuni, Twamjua Yeye Mlinzi aliye karibu sana. 4. Mungu wetu Ficho kwetu, kimbilio taabuni, Siku zote uwe Boma lililo karibu sana. (Amina)